Mathayo 13 SWHULB
Mathayo Chapter 13 SWHULB Bible Verse Images
Copyright © 2019 Door43 World Missions Community
Language: Kiswahili (Swahili)
Translation by: Door43 World Missions Community
Contributors: Alfred Danjuma, Bariki Malisa, Christina Abraham Kileo, Cloud Roman, Daniel Marura Chacha, Dina Mast, Dina Roman, Donald Shadarck Dutuyi, Emmanuel Masanja Mbaaga, Emmanuel Nyamalya, Erasmus Peter Malelo, Ev. Lazaro Chalomhola, Ezekiel Manala, Fred, Gabriel Gidale Merus, Gabriel Lwitakubi Mazige, James Makula, James Semnkai, Jeremiah Masasi, Jesse Katabi Masolwa, John Ojasi, Joyce Gilbert Masasi, Karen Riecks, Kazwanomo, Kennedy, Ker, Lameck Yakobo Tobotobo, Laurent Petro Malelo, Lazarus David Chalomhola, Makene Mafwele, Marco Luma Mahushi, Mathew Nkusa, Mathias William, Mr. James Semnkai .It., Musa Isaya Majama, Musa Luzali, Pastor John Kerim, Pastor Jordan, Philipo Mussa Kanwelle, Raphael Musa, Rev. Charles Mabisa, Rev. Yohana Batano, Robert Ndalahwa, Sadiki Kulwa, Samson Nungwana, Thobias Kazwanomo, Yohana Dutuyi, Yohana Magera, Zelote Loilang'akaki Lukumay, Rev. Erasmus Peter Malelo, Ev. Mathew Kazimoto, Rev. Dr. David Magoke, Rev. Elias Ndema, Rev. Alex Nyuri, Rev. Gungutu Elias, Rev. Lameck Tobotobo, Rev. Catherin D. Matia, Rev. Yohana S Dutuyi, Rev. Donald Dutuyi, GS. Andrew Gewe, Ev. Ezekiel Daudi, Rev. John Ndaluka, Ev. Moses Malugu, Rev. Moses Eliakim Ndege, Past. Isack A. Gomugo, Past. Mathias William, Rev. Yekonia M. Koko, Rev. Elisande Mhanga, Ev. James A. Makula.
This translation is made available to you under the terms of the Creative Commons Attribution Share-Alike license 4.0.
You have permission to share and redistribute this Bible translation in any format and to make reasonable revisions and adaptations of this translation, provided that:
- You include the above copyright and source information.
- If you make any changes to the text, you must indicate that you did so in a way that makes it clear that the original licensor is not necessarily endorsing your changes.
- If you redistribute this text, you must distribute your contributions under the same license as the original.
Credits: In addition, we would like to give very special thanks to eBible.org for making Swahili Unlocked Literal Bible available in MySQL format.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Katika siku hiyo Yesu aliondoka nyumbani na kukaa kando ya bahari.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Umati mkubwa ulikusanyika kwa kumzunguka, aliingia ndani ya mtumbwi na kukaa ndani yake. Umati wote walisimama kando ya bahari.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha Yesu alisema maneno mengi kwa mifano, Alisema, “Tazama, mpanzi alienda kupanda.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Alipokuwa akipanda baadhi ya mbegu zilianguka kando ya njia na ndege walikuja wakazidonoa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mbegu zingine zilianguka juu ya mwamba, ambapo hazikupata udongo wa kutosha. Ghafla zilichipuka kwa sababu udongo haukuwa na kina.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini jua lilipo chomoza zilichomwa kwa sababu hazikuwa na mizizi, na zilikauka.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mbengu zingine zilianguka kati ya miti yenye miiba. Miti yenye miiba ilirefuka juu ikaisonga.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mbegu zingine zilianguka kwenye udongo mzuri na kuzaa mbegu, zingine mara mia moja zaidi, zingine sitini na zingine thelathini
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wanafunzi walikuja na kumwambia Yesu, “Kwa nini unazungumza na makutano kwa mifano?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu alijibu kuwaambia, “Mmepewa upendeleo wa kufahamu siri za ufalme wa mbinguni, bali kwao hawajapewa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini yeyote aliyenacho, kwake yeye ataongezewa zaidi, na atapata faida kubwa. Ilasiye nacho hata kile alichonacho atanyang'anywa. .
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hivyo naongea nao kwa mifano kwa sababu ingawa wanaona, wasione kweli. Na ingawa wanasikia wasisikie wala kufahamu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Unabii wa Isaya umetimia kwao, ule usemao, “Msikiapo msikie, lakini kwa namna yoyote hamtaelewa; wakati mwonapo muweze kuona, lakini kwa namna yeyote ile msijue.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na mioyo ya watu hawa imekuwa giza, ni vigumu kusikia, na wamefumba macho yao, ili wasiweze kuona kwa macho yao, au kusikia kwa masikio yao, au kufahamu kwa mioyo yao, hivyo wangenigeukia tena, na ningewaponya.'
Square Portrait Landscape 4K UHD
Bali macho yenu yamebarikiwa, kwa kuwa yanaona, na masikio yenu kwa kuwa yanasikia.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hakika nawaambia manabii wengi na watu wenye haki walikuwa na hamu ya kuyaona mambo yale myaonayo, na hawakuweza kuyaona. Walitamani kusikia mambo yale mnayosikia, hawakuyasikia.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakati yeyote asikiapo neno la ufalme na asilifahamu, ndipo mwovu huja na kukinyakua kilichokwisha kupandwa ndani ya moyo wake. Hii ni mbegu ile iliyopandwa kando ya njia.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yeye aliyepandwa katika miamba ni yule asikiaye neno na kulipokea haraka kwa furaha.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Bado hana mizizi ndani yake, ila huvumilia kwa kitambo kifupi. Wakati matatizo au mateso yanapotokea kwa sababu ya neno hujikwaa ghafla.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Aliyepandwa kati ya miti ya miiba, huyu ni yule alisikiaye neno lakini masumbuko ya ulimwengu na udaganyifu wa utajiri hulisonga lile neno lisije likazaa matunda.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Aliyepandwa kwenye udongo mzuri, huyu ni yule asikiaye neno na kulifahamu. Huyu ni yule azaaye matunda na kuendelea kuzaa moja zaidi ya mara mia, nyingine sitini, nyingine thelathini.''
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu aliwapa mfano mwingine. Akisema, “Ufalme wa mbinguni unafananishwa na mtu aliye panda mbengu nzuri katika shamba lake
Square Portrait Landscape 4K UHD
Lakini watu waliposinzia, adui wake akaja pia akapanda magugu katikati ya ngano kisha akaenda zake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Baadaye ngano ilipoota na kutoa mazao yake, ndipo magugu yalitokea pia.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na watumishi wa mwenye shamba walikuja wakamwambia, 'Bwana, hukupanda mbengu nzuri katika shamba lako? Imekuwaje sasa lina magugu?
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akawaambia, Adui ametenda hili.' Watumishi walimwambia, “Kwa hiyo unataka twende tukayang'oe?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mwenye shamba akisema, 'Hapana, wakati mnayang'oa magugu mtang'oa pamoja na ngano.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yaacheni yakue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati wa mavuno nitasema kwa wavunaji, 'Kwanza yang'oeri magugu na yafungeni matita matita na kuyachoma, lakini kusanyeni ngano katika ghala langu.''''
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha Yesu aliwatolea mfano mwingine. Akasema, “Ufalme wa mbinguni unafanana na mbegu ya haradali ambayo mtu aliichukua na kuipanda katika shamba lake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mbegu hii kwa hakika ni ndogo kuliko mbegu zingine zote. Lakini imeapo huwa kubwa kuliko mimea yote ya bustani, huwa mti, kiasi kwamba ndege wa angani huja na kujenga viota katika matawi yake.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Akawaambia mfano mwingine tena.”Ufalme wa mbinguni ni kama chachu ile iliyo twaliwa na mwanamke na kuichanganya kwa vipimo vitatu kwa unga mpaka viumuke.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hayo yote Yesu aliyasema kwenye umati kwa mifano. Na pasipo mifano hakusema chochote kwao.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hii ilikuwa kwamba kile kilichokwisha semwa kupitia kwa nabii kiweze kutimia, pale aliposema, “Nitafumbua kinywa changu katika mifano. Nitasema mambo yale yaliyokuwa yamefichwa tangu misingi ya ulimwengu”.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha Yesu aliwaacha makutano na kwenda nyumbani. Wanafunzi wake walimwendea na kusema, “Tufafanulie mfano wa magugu ya shambani.''
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu alijibu na kusema, “Apandae mbegu nzuri ni Mwana wa Adamu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Shamba ni ulimwengu; na mbegu nzuri, hawa ni wana wa ufalme. Magugu ni wana wa yule mwovu, na adui aliye zipanda ni ibilisi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na mavuno ni mwisho wa ulimwengu, na wavunaji ni malaika.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kama vile magugu yanavyo kusanywa na kuchomwa moto, hivyo ndivyo itakavyo kuwa mwisho wa ulimwengu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mwana wa Adamu atatuma malaika wake, na kukusanya kutoka katika ufalme wake mambo yote yaliyosababisha dhambi na wale watendao maasi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Watawatupa wote katika tanuru la moto, ambako kutakuwa na kilio na kusaga meno.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ndipo watu wenye haki watakapong'aa kama jua katika Ufalme wa Baba yao. Yeye aliye na masikio na sikie.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ufalme wa mbinguni ni kama hazina iliyofichwa shambani. Mtu akaiona na kuificha. Katika furaha yake akaenda kuuza vyote alivyokuwa navyo, na kulinunua shamba.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Tena, ufalme wa mbinguni ni kama mtu anayefanya biashara atafutaye lulu yenye thamani.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wakati alipoiona ile yenye thamani, alienda akauza kila kitu alichokuwa nacho na akainunua.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ufalme wa mbinguni ni kama nyavu iliyo ndani ya bahari, na kwamba hukusanya viumbe vya kila aina.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ulipojaa wavuvi waliuvuta ufukweni. Kisha wakakaa chini wakakusanya vitu vyema ndani ya vyombo, lakini visivyo na thamani vilitupwa mbali.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Itakuwa namna hii katika mwisho wa dunia. Malaika watakuja na kuwatenga watu waovu kutoka miongoni mwa wenye haki.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na kuwatupa ndani ya tanuru ya moto, ambako kutakuwa na maombolezo na kusaga meno.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mmefahamu mambo yote haya? Wanafunzi walimjibu, ''Ndiyo.''
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha Yesu akawambia, ''Kila mwandishi ambaye amekuwa mwanafunzi wa ufalme anafanana na mwenye nyumba atoaye katika hazina yake vitu vipya na vya kale.''
Square Portrait Landscape 4K UHD
IkawaYesu alipomaliza mifano yote hiyo, akaondoka katika sehemu hiyo.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha Yesu akafika katika mkoa wake na akawafundisha watu katika sinagogi. Matokeo yake ni kuwa walishangaa na kusema, “Ni wapi mtu huyu alipopata hekima hii na miujiza hii?
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mtu huyu siyo mwana wa seremala? Mariamu siyo mamaye? Na ndugu zake siyo Yakobo, Yusuph, Simoni na Yuda?
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na dada zake tunao hapa petu? Basi mtu huyu ameyapata wapi haya yote?”.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Aliwachukiza. Lakini Yesu aliwambia, “Nabii hakosi kuwa na heshima isipokuwa kwao na katika nchi yao.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na hakuweza kufanya miujiza mingi kwa sababu hawakuwa na imani naye.
Available Bible Translations
Matthew 13 (ASV) »
Matthew 13 (KJV) »
Matthew 13 (GW) »
Matthew 13 (BSB) »
Matthew 13 (WEB) »
Matthieu 13 (LSG) »
Matthäus 13 (LUTH1912) »
मत्ती 13 (HINIRV) »
ਮੱਤੀ 13 (PANIRV) »
মথি 13 (BENIRV) »
மத்தேயு 13 (TAMIRV) »
मत्तय 13 (MARIRV) »
మత్తయి 13 (TELIRV) »
માથ્થી 13 (GUJIRV) »
ಮತ್ತಾಯನು 13 (KANIRV) »
مَتَّى 13 (AVD) »
הבשורה על־פי מתי 13 (HEB) »
Mateus 13 (BSL) »
Ma-thi-ơ 13 (VIE) »
Mateo 13 (RVA) »
Matteo 13 (RIV) »
马 太 福 音 13 (CUVS) »
馬 太 福 音 13 (CUVT) »
Mateu 13 (ALB) »
Matteus 13 (SV1917) »
Матфея 13 (RUSV) »
Матвія 13 (UKR) »
Máté 13 (KAR) »
Матей 13 (BULG) »
マタイによる福音書 13 (JPN) »
Matteus 13 (NORSK) »
Mateusza 13 (POLUBG) »
Matayos 13 (SOM) »
Mattheüs 13 (NLD) »
Matthæus 13 (DA1871) »