Yohana 12 SWHULB
Yohana Chapter 12 SWHULB Bible Verse Images
Copyright © 2019 Door43 World Missions Community
Language: Kiswahili (Swahili)
Translation by: Door43 World Missions Community
Contributors: Alfred Danjuma, Bariki Malisa, Christina Abraham Kileo, Cloud Roman, Daniel Marura Chacha, Dina Mast, Dina Roman, Donald Shadarck Dutuyi, Emmanuel Masanja Mbaaga, Emmanuel Nyamalya, Erasmus Peter Malelo, Ev. Lazaro Chalomhola, Ezekiel Manala, Fred, Gabriel Gidale Merus, Gabriel Lwitakubi Mazige, James Makula, James Semnkai, Jeremiah Masasi, Jesse Katabi Masolwa, John Ojasi, Joyce Gilbert Masasi, Karen Riecks, Kazwanomo, Kennedy, Ker, Lameck Yakobo Tobotobo, Laurent Petro Malelo, Lazarus David Chalomhola, Makene Mafwele, Marco Luma Mahushi, Mathew Nkusa, Mathias William, Mr. James Semnkai .It., Musa Isaya Majama, Musa Luzali, Pastor John Kerim, Pastor Jordan, Philipo Mussa Kanwelle, Raphael Musa, Rev. Charles Mabisa, Rev. Yohana Batano, Robert Ndalahwa, Sadiki Kulwa, Samson Nungwana, Thobias Kazwanomo, Yohana Dutuyi, Yohana Magera, Zelote Loilang'akaki Lukumay, Rev. Erasmus Peter Malelo, Ev. Mathew Kazimoto, Rev. Dr. David Magoke, Rev. Elias Ndema, Rev. Alex Nyuri, Rev. Gungutu Elias, Rev. Lameck Tobotobo, Rev. Catherin D. Matia, Rev. Yohana S Dutuyi, Rev. Donald Dutuyi, GS. Andrew Gewe, Ev. Ezekiel Daudi, Rev. John Ndaluka, Ev. Moses Malugu, Rev. Moses Eliakim Ndege, Past. Isack A. Gomugo, Past. Mathias William, Rev. Yekonia M. Koko, Rev. Elisande Mhanga, Ev. James A. Makula.
This translation is made available to you under the terms of the Creative Commons Attribution Share-Alike license 4.0.
You have permission to share and redistribute this Bible translation in any format and to make reasonable revisions and adaptations of this translation, provided that:
- You include the above copyright and source information.
- If you make any changes to the text, you must indicate that you did so in a way that makes it clear that the original licensor is not necessarily endorsing your changes.
- If you redistribute this text, you must distribute your contributions under the same license as the original.
Credits: In addition, we would like to give very special thanks to eBible.org for making Swahili Unlocked Literal Bible available in MySQL format.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Siku sita kabla ya Pasaka, Yesu alienda Bethania, alipokuwapo Lazaro, yeye ambaye alimfufua kutoka katika wafu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Basi wakamwandalia chakula cha jioni huko, na Martha akamtumikia, wakati huo Lazaro alikuwa mmoja wapo wa wale walioketi chakulani pamoja na Yesu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Kisha Mariamu akachukua ratli ya manukato yaliyotengenezwa kwa nardo safi, yenye thamani kubwa, akampaka Yesu miguuni, na kumfuta miguu kwa nywele zake; nyumba yote ilijaa harufu ya manukato.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yuda Iskariote, mmoja wa wale wanafunzi wake, ambaye ndiye atakayemsaliti Yesu, akasema,
Square Portrait Landscape 4K UHD
“Kwanini manukato haya yasingeuzwa kwa dinari mia tatu na wakapewa maskini?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Naye aliyasema hayo, si kwa kuwahurumia maskini, bali kwa sababu alikuwa mwizi: yeye ndiye aliyeshika mfuko wa fedha na alikuwa anachukua baadhi ya vilivyowekwa humo kwa ajili yake mwenyewe.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu alisema, “Mwache aweke alicho nacho kwa ajili ya siku ya maziko yangu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Maskini mtakuwa nao siku zote; lakini hamtakuwa nami siku zote.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Basi umati mkubwa wa Wayahudi walipata kujua ya kuwa Yesu yuko huko, nao wakaja, si kwa ajili ya Yesu tu, ila wamwone na Lazaro ambaye Yesu alimfufua kutoka katika wafu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Nao wakuu wa makuhani wakafanya shauri ili wamue Lazaro;
Square Portrait Landscape 4K UHD
maana kwa ajili yake wengi katika Wayahudi walienda zao na wakamwamini Yesu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na siku ya pili yake umati mkubwa walikuja kwenye sikukuu. Waliposikia ya kuwa Yesu anakuja Yerusalemu,
Square Portrait Landscape 4K UHD
walichukua matawi ya miti ya mitende na kutoka nje kwenda kumlaki na wakapiga kelele, “Hosana! Amebarikiwa yeye ajaye kwa jina la Bwana, Mfalme wa Israeli.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu alimpata mwana-punda akampanda; kama vile ilivyoandikwa,
Square Portrait Landscape 4K UHD
“Usiogope, binti Sayuni; tazama, Mfalme wako anakuja, amepanda mwana-punda.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Wanafunzi wake hawakuyaelewa mambo haya hapo kwanza; lakini Yesu alipotukuzwa, ndipo walipokumbuka ya kuwa mambo haya aliandikiwa yeye na ya kwamba wametenda mambo haya kwake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Basi lile kundi la watu waliokuwepo pamoja na Yesu wakati alipomwita Lazaro kutoka kaburini, wakashuhudia kwa wengine.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Na ilikuwa kwa sababu hii pia kwamba kundi la watu walikwenda kumlaki kwasababu walisikia ya kwamba ameifanya ishara hiyo.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mafarisayo wakasemezana wao kwa wao, “Tazama, sasa hamwezi kufanya lolote; tazama, ulimwengu umekwenda kwake.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Sasa baadhi ya Wayunani walikuwa miongoni mwa wale waliokuwa wakienda kuabudu kwenye sikukuu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Hawa walimwendea Filipo, ambaye alitoka Bethsaida ya Galilaya, wakamwomba wakisema, “Bwana, sisi tunatamani kumwona Yesu.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Filipo akaenda akamwambia Andrea; Andrea na Filipo wakaenda na kumwambia Yesu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akawajibu akasema, “Saa imefika kwa ajili ya Mwana wa Adamu kutukuzwa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Amini, amini, nawaambia, chembe ya ngano isipoanguka katika nchi ikafa, hukaa hali iyo hiyo peke yake; bali ikifa, itazaa matunda mengi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yeye apendaye uhai wake ataupoteza; bali yeye auchukiaye uhai wake katika ulimemngu huu atausalimisha hata uzima wa milele.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mtu yeyote akinitumikia mimi, na anifuate; nami nilipo, ndipo na mtumishi wangu atakapokuwapo. Mtu yeyote akinitumikia, Baba atamheshimu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Sasa roho yangu imefadhaika: nami nisemeje? 'Baba, uniokoe katika saa hii'? Lakini ni kwa kusudi hii nimeifikia saa hii.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Baba, ulitukuze jina lako.” Kisha sauti ikaja kutoka mbinguni na kusema, “Nimelitukuza nami nitalitukuza tena.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Basi mkutano uliosimama karibu naye wakasikia, wakasema ya kwamba kumekuwa ngurumo. Wengine walisema, “Malaika amesema naye.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akajibu na kusema, “Sauti hii haikuja kwa ajili yangu, bali kwa ajili yenu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Sasa hukumu ya ulimwengu huu ipo: Sasa mkuu wa ulimwngu huu atatupwa nje.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Nami nikiinuliwa juu ya nchi, nitawavuta wote kwangu.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Aliyanena hayo akionesha ni mauti gani atakayokufa.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mkutano wakamjibu, “Sisi tumesikia katika sheria ya kwamba Kristo atadumu hata milele. Nawe wasemaje, 'Mwana Adamu lazima ainuliwe juu'? Huyu Mwana wa Mtu ni nani?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Basi Yesu akawaambia, “Nuru ingalipo pamoja nanyi muda kidogo. Enendeni maadamu mnayo nuru, ili kwamba giza lisije likawaweza. Yeye aendaye gizani hajui aendako.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mngali mnayo nuru, iaminini nuru hiyo ili mpate kuwa wana wa nuru.” Yesu aliyasema haya na kisha akaenda zake akajificha wasimwone.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ingawa Yesu alifanya ishara nyingi namna hiyo mbele yao, bado hawakumwamini
Square Portrait Landscape 4K UHD
ili litimie neno la nabii Isaya, alilosema: “Bwana, ni nani aliyezisadiki habari zetu? Na mkono wa Bwana amefunuliwa nani?”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ndio sababu wao hawakuamini, maana Isaya alisema tena,
Square Portrait Landscape 4K UHD
“Amewapofusha macho, na ameifanya migumu mioyo yao; wasije wakaona kwa macho yao na wakafahamu kwa mioyo yao, na wakaongoka nami nikawaponya.”
Square Portrait Landscape 4K UHD
Isaya alisema maneno hayo kwa kuwa aliuona utukufu wa Yesu na akanena habari zake.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walakini, hata wakuu wengi walimwamini Yesu; lakini kwa sababu ya Mafarisayo, hawakukiri ili wasije wakatengwa na sinagogi.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Walipenda sifa za wanadamu kuliko sifa zitokazo kwa Mungu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yesu akapaza sauti na kusema, “Yeye aniaminiye mimi, haniamini mimi tu bali na yeye aliyenituma mimi,
Square Portrait Landscape 4K UHD
naye anionaye mimi anamuona yeye aliyenituma.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Mimi nimekuja kama nuru ulimwenguni ili kila mtu aniaminiye mimi asikae gizani.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Ikiwa mtu yeyote atayasikia maneno yangu lakini asiyashike, mimi simhukumu; maana sikuja ili niuhukumu ulimwengu, bali niuokoe ulimwengu.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Yeye anikataye mimi na asiyeyakubali maneno yangu, anaye amhukumuye: neno hilo nililolinena ndilo litakalomhukumu siku ya mwisho.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Maana mimi sikunena kwa nafsi yangu tu. Bali ni Baba aliyenipeleka, yeye mwenyewe ameniagiza nitakayonena na nitakayosema.
Square Portrait Landscape 4K UHD
Nami najua ya kuwa agizo lake ni uzima wa milele; basi hayo ninenayo mimi - kama Baba alivyoniambia, ndivyo ninenavyo kwao.”
Available Bible Translations
John 12 (ASV) »
John 12 (KJV) »
John 12 (GW) »
John 12 (BSB) »
John 12 (WEB) »
Jean 12 (LSG) »
Johannes 12 (LUTH1912) »
यूहन्ना 12 (HINIRV) »
ਯੂਹੰਨਾ 12 (PANIRV) »
যোহন 12 (BENIRV) »
யோவான் 12 (TAMIRV) »
योहान 12 (MARIRV) »
యోహాను 12 (TELIRV) »
યોહાન 12 (GUJIRV) »
ಯೋಹಾನನು 12 (KANIRV) »
يوحنَّا 12 (AVD) »
הבשורה על־פי יוחנן 12 (HEB) »
João 12 (BSL) »
Giăng 12 (VIE) »
Juan 12 (RVA) »
Giovanni 12 (RIV) »
约 翰 福 音 12 (CUVS) »
約 翰 福 音 12 (CUVT) »
Gjoni 12 (ALB) »
Johannes 12 (SV1917) »
Иоанна 12 (RUSV) »
Івана 12 (UKR) »
János 12 (KAR) »
Йоан 12 (BULG) »
ヨハネによる福音書 12 (JPN) »
Johannes 12 (NORSK) »
Jana 12 (POLUBG) »
Yooxanaa 12 (SOM) »
Johannes 12 (NLD) »
Johannes 12 (DA1871) »